DUUH…! JAMANI MSIMCHUKULIE HIVYO HARMONIZE.
MKALI toka lebo ya Wasafi Clasic Baby ‘WCB’ iliyo chini ya
mtu mzima Diamond Platnum ‘SIMBA’ Rajabu
Ibrahimu ‘Harmonize’ amekanusha uvumi unao enea kuwa yeye ni msanii anaye jiona na kujivuna,
kwa kutaja sababu mbalimbali kama yeye kuwa bize na shughuli zake zinazo mfanya
asitokee mbele ya watu wengi mara kwa mara.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, nyota huyo anayetamba na
ngoma ya ‘Niambie’, amesema kuwa muda wake mwingi huwa anautumia studio,
akitoka studio anaelekea Kunduchi kwa mama yake, akitoka huko huwa anaelekea
Kijito nyama kwa Jack, hivyo hiyo ndiyo ratiba yake.
“So nikiwa nyumbani nina Gym, ofisini nafanya project zangu,
kwa Baby nina relax, hivyo sinaga hizo mambo, na ndio maana watu wanahisi labda
ninajivuna sababu sitokei sehemu za watu wengi. Amesema Harmonize.
Harmonize pia amekiri kuwa yeye ni moja kati ya wasanii
walio pitia maisha magumu yaliyo mfanya awe na heshima kwa kila mtu hivyo
hawezi kuwa na dharau kwa kujiona au kujivuna.
“Japokuwa kueleza shida zako si vizuri, lakini unaweza ukawa’inspire’
watu tofauti, hivyo nimepitia shida nyingi sana na nina mheshimu kila mtu na
sina dharau sababu ninaiogopa kesho yangu kwakuwa siijuwi na sijuwi nani
atakaye nisaidia.” alisema Harmonize.
No comments