MLIOKUWA KATIKA MFUNGO MSIKILIZENI IDRIS
Na.Melkiory
Gowelle.
MTANGAZAJI na msanii wa vichekesho
nchini Idriss Sultan amewataka waislamu wote kuswali sana na kufanya vitu
vinavyompendeza Mwenyez Mungu ili awashushie neema.
Akizungumza Jijini dar es salaam
Idris amesema majaribu ni mengi hasa katika kipindi cha Ramadhani na wakati
mwingine hivyo amewataka kufanya mema ili waifikie pepo.
"Katika mafundisho ya dini kwa
ujumla Waislamu haturuhusiwi kusikiliza miziki ya kidunia hasa kipindi cha
Ramadhani na vipindi vya kawaida, lakini cha ajabu waislamu wengi ndio tunao
imba na kuisikiliza miziki hiyo, hivyo sidhani kama tutaiona pepo pasipo
kujitahidi kuswali na kufuata mafundisho ya dini." amesema Idris.
Aidha Idris ameeleza kitu ambacho
kwa upande wake hapendi kukifanya katika kipindi cha Ramadhani ikiwezekana pia
katika vipindi vingine ni kujihusisa na mahusiano ya kimapenzi bila kuoa.
"Haturuhusiwi kidini kuwa na
mahusiano bila kuoa, lakini kuna waislamu wanaamini haturuhusiwi kufanya
mapenzi wakati wa Ramadhani, mimi nasema hapana, Mwenyezi Mungu hajasema
Ramadhani peke yake bali ni kila siku". amesema Idris.
No comments