NI TOX STAR NA BELL9 KATIKA BIFU ZITO
Na.Melkiory Gowelle
MSANII wa Bongo fleva nchini Tox
star amelalamikia kitendo kilicho fanywa na msanii mwenzake Bell9 kutumia
mashairi ya ngoma yake iitwayo 'Ole' pasipo makubaliano kati yao.
Akizungumza Jijini dar es salaam Tox
star amesema asilimia 70℅ ya ngoma ya Bell9 ijulikanayo kama 'Maole' ni kopi ya
Ole iliyo rekodiwa mwaka 2014.
"Chorus wameimba kama
nilivyoimba mimi, walicho kifanya wao ni kupunguza speed ya uimbaji lakini
chorus, mashairi mpaka melody wamefanya kama nilivyo fanya mimi.alisema Tox na
kuongeza
"Wamekopi mpaka jina la wimbo
sababu mimi nimeuita Ole wao wameuita Maole, sawa leo na mimi nitoe ngoma alafu
niuite Mamasogange." alisema Tox.
Kuhusu kumalizana na Belle9 mkali
huyo aliyewahi kutamba na ngoma yake ya Pretty girl amesema hana muda wa kumtafuta
Bell9 wala uongozi wake.
"Mimi siwezi nikamtafuta
kwasababu wao ndio wenye makosa hivyo wao ndio watakiwa wanitafute mimi".
alisema Tox.
No comments