NEY WA MITEGO AWATETEA POLISI, AWATAKA RAIA KUFANYA HAYA.
MKALI wa Hip hop nchini mwenye staili ya makavu
live, Emanuel Elibariki ‘Ney wa mitego’ amesema kuwa hawezi kulaumu Jeshi la
Polisi kwa kitendo cha kumkamata na kumlaza Lumande, kwasababu anatambuwa kuwa
Jeshi hilo lilikuwa linatekeleza majukumu yake.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mjini Dodoma mara
baada ya kuitika wito na kumaliza mazungumzo rasmi na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dakta Harrison Mwakyembe, Ney amewataka Raia wote
wa Tanzania kuheshimu majukumu yanayo tekelezwa na Jeshi hilo.
“Najuwa wengi watakuwa wanajiuliza kwanini Ney
amekamatwa wakati ni mtu maarufu ambaye angeambiwa afike kituo cha polisi angefika
mara moja, hivyo raia tusilitumie vibaya Jeshi la Polisi kwa kuwachukia pindi
wanapo tekeleza majukumu yao.” Alisema Ney.
Ney alikamatwa na Polisi mara baada ya kusambaa kwa
wimbo wake wa ‘WAPO’ katika mitandao ya kijamii ambao unasheheni mistari tata
inayo kashifu Serikali ya Rais Magufuli, na aliachiwa kwa ruhusa ya Rais na
aliitwa na Waziri mwenye dhamana ya sanaa kwa ajili ya mazungumzo juu ya wimbo
huo.
Kwa upande wake Dakta Mwakyembe amesema wameelewana
na msanii huyo na anasubiri nakala ya Remix ya wimbo huo ambapo anaamini
itakuwa nzuri zaidi na akiipata atamfikishia Mh.Rais kwa kuwa nay eye ametokea
kuupenda wimbo huo.
No comments