ROSE NDAUKA KUJA NA TAMTHILIYA
Na. Melkiory Gowelle.
NYOTA wa filamu nchini kutoka Kampuni ya Ndauka
Entertainment Rose Ndauka, amesema yuko mbioni kuachia tamthiliya mpya ambapo
kwa sasa anaifanyia maandalizi.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Ndauka amewataka
Wapenzi na Mashabiki wake kukaa mkao wa kula na atawapa taarifa rasmi wakati
muafaka utakapo fika.
“Niko mbioni kuachia ‘Series’, hicho ndicho kitu
kipya na lazima nitawajulisha Watanzania kwamba tayari kuna kitu kipya, lini
kitatoka, na nani atakuwepo hivyo vyote nitawajulisha muda na wakati muafaka
utakapo fika.” Alisema Ndauka.
Ndauka ni mmoja kati ya Wasanii wa filamu ambao
nyota zao zilianza kung’aa tangu wakiwa wadoga ambapo alifanikiwa kuigiza
filamu yake ya kwanza ya ‘SWAHIBA’ mwaka 2007 wakati akiwa bado anasoma shule
ya Sekondari Zanaki Dar es salaam.
No comments