BASATA WAMEBARIKI MADARAKA YA KULEVYA
Na. Melkiory Gowelle.
MKALI wa Hip hop Bongo kutoka katika kundi la Weusi
John Simon ‘Joh Makini’ amesema kuwa wimbo wao mpya ulio sheheni mistari mingi
yenye maneno ya kisasa ujulikanao kama Madaraka ya kulevya umekaguliwa na
BARAZA LA SANAA TANZANIA ‘BASATA’ na kupewa ruhusa ya kuchezwa katika media
mbalimbali.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akitoa
ufafanuzi wa maudhui ya wimbo huo ambapo amesema wimbo huo unahusu Mapenzi na
unamzungumzia Mwanaume ambaye amependwa sana na mke wake.
“Wimbo tuliuita Yakulevya, lakini watu wengi
hawakuuelewa sababu kabla ya kuutoa tuliachia ‘sample’ ya ‘choras’ ambayo kila
mtu aliipokea kwa maana yake na kuu’brand’ kama madaraka ya kulevya. Hivyo kwakuwa
hauwezi kuwazuia mashabiki basi tukaacha uitwe hivyo Madaraka ya kulevya.” Alisema
Joh.
Kuhusu BASATA Joh amefafanua kuwa sikuizi kuna
utaratibu wa kuifikisha nyimbo kwa Baraza hiyo kabla haujaachiwa kwenye media,
hivyo walifuata utaratibu huo ndipo wimbo huo ukapewa ruhusa ya kuchezwa katika
media mbalimbali.
“Tuliupeleka wimbo BASATA na wakaupokea, wakausikia
na wakaukubali na kusifia ubunifu wa sanaa iliyo tumika, hivyo kwa mikono
miwili wameibariki na kutoa ‘go ahead’. Amesema Joh.
No comments