IGP AHAIDI KUKOMESHA VITENDO VYA UHALIFU PWANI.
Na.Melkiory Gowelle.
MARA baada ya kuapishwa na kuwa IGP aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro amesisitiza kwamba
suala la mauaji linaloendelea maeneo ya Mkoani Pwani litakoma mara moja na kuwafanya Wana pwani kuishi kwa
amani na utulivu.
Akizungumza Ikulu Jijini Dar es salaam IGP Sirro
amesema kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda Raia na mali zao, hivyo
amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano ili kukabiliana na kasi ya uhalifu
nchini.
“Uhalifu hauwezi ukapunguwa kwa kutegemea Jeshi la
Polisi peke yake, tunahitaji nguvu ya pamoja ili kushinda hii vita. Amesema Sirro
na kuongeza kuwa
“Najuwa tunachangamoto kubwa ya Ikwiriri, Rufiji na
maeneo mengine ya Pwani lakini Jeshi la polisi tuko vizuri, na tutaingia, tutafanyia
kazi kuhakikisha Wanapwani wanaishi kwa amani na utulivu, lakini watuamini na
watupe taarifa kwa kuwa ‘information is
power’.” Amesema Sirro.
Kwa upande wake aliyekuwa katika nafasi hiyo IGP Ernest Mangu amemuunga mkono
Sirro na kuwataka wananchi kumpa ushirikiano ili aweze kukabiliana na majukumu yak
e kwa ufanisi.
“IGP mpya sio mgeni ndani ya Jeshi la Polisi, na
alikuwa katika nafasi ya juu hivyo anaelewa changamoto zilizo kuwepo na hatuwa
za kuchukuwa , naamini amejipanga kwa ajili ya kukabiliana na uhalifu ambao
hatuja wahi kuushuhudia nchini kwetu.” Amesema Mangu.
No comments