bana

bana

MBARAKA KUMBE HANA NOMA NA SIMBA, ASEMA YUKO TAYARI KURUDI LAKINII….

Na.Melkiory Gowelle.




YULE kinda matata na mfungaji bora wa Kagera Sugar 2016/2017 Mbaraka Yusuph amesema yuko tayari kurudi Simba ikiwa Wekundu hao wa Msimbazi watakubali kumtimizia anacho kitaka.

Mbaraka amesema kuwa timu zote kubwa za Ligi kuu bara VPL, zimeonyesha nia ya kuinasa saini yake ili kufanya nae kazi kwa msimu ujao 2017/2018.

“Timu nyingi zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yangu ikiwemo Kagera Sugar, Simba, Yanga, Azam na Singida united na nipo tayari kuitumikia timu yeyote kama watakubaliana na masharti yangu.” Amesema Mbaraka.

Akizungumzia suala la utata ulio ibuka kati yake, Simba na Kagera Sugar, Mbaraka amesema ile ni mbinu ya Simba kumshusha morali ya mchezo ili asiwanie nafasi ya ufungaji bora.

“Namshukuru kocha kwakuwa alinitia moyo na kunitaka nizidi kupambana kwa kuniambia kila kitu kitakuwa sawa, lakini katika utata ule Kagera Sugar walikuwa sahihi kusema mimi ni mchezaji wao. Alisema Mbaraka.


Mbaraka ni mmoja kati ya wachezaji walio tokea katika kikosi cha pili cha Simba kabla ya kutuwa Kagera Sugar, lakini hivi sasa ndiye mchezaji anayeshikiria tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa ‘VPL’ 2016/2017 akiwa ndani ya kikosi cha Wana nkurukumbi ‘Kagera Sugar’.    

No comments

Powered by Blogger.