MANULA: HATA SAMATTA AKIKOSEKANA USHINDI UPO NDANI YA STARS
Na. Melkiory Gowelle.
MLINDA mlango namba moja wa Azam Sc na timu ya Taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Aishi Manula
amesema kuwa kutokana na maendeleo ya Soka nchini hakuta kuwa na mfungaji tegemezi
katika kikosi cha Taifa Stars.
Akizungumza Jijini dar es salaam Manula ameeleza
sababu kubwa ya yeye kusema hivyo ni kuibuka kwa kasi ya ‘mastreika’ wa ndani kufanya
vizuri zaidi katika nafasi ya ufungaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
“Ni kitu kizuri sana katika nchi yetu na ukiangalia,
ukiangalia misimu ya hivi karibuni nafasi hii ilikuwa inawaniwa na wachezaji wa
kigeni kitu ambacho kili ibuwa kelele
nyingi zilizo semza hatuna wafungaji katika nchi yetu. Alisema Manula na
kuongeza kuwa
“Walikuwa wanaamini ya kwamba tukimtoa samatta basi hatuna mfungaji mwingine, lakini ujio wa
Msuva, Kichuya, Abrahaman, na wengine
wengi umeleta imani ya hata tukicheza bila Samatta tunaweza kufunga.” Alisema Manula.
Mwisho Manula amewapongeza wachezaji wote walio
chukuwa tuzo ya mfungaji bora VPL 2016/2017
na waliokuwa wakiwania tuzo hiyo na kuwataka waongeze juhudi zaidi ili waweze
kuisaidia timu yao ya Taifa Stars.
No comments