AC MILANI RASMI KWENYE MIKONO YA WACHINA
Timu ya kandanda ya AC Milan ya Italia imeuziwa kampuni moja ya Uchina na kutia kikomo umiliki wake na aliyekuwa wakati mmoja Waziri Mkuu wa nchi hiyo na tajiri Silvio Berlusconi.
Kampuni ya China Rossoneri Sport Investment Lux, imekamilisha mkataba wa kuinunua timu hiyo kwa kima cha dola milioni 628, huku ikiwa na matumaini ya "kuongeza faida mara dufu".
Klabu hiyo ya Serie A imekuwa chini ya umiliki wa bilionea Silvio Berlusconi, tangu mwaka 1986.
Katika kipindi hicho chote, AC Milan ilifaulu kunyakua mataji manane katika ligi kuu na kunyakuwa kombe la vilabu bingwa barani Ulaya mara tano.
Aidha, Milan haijawahi kushinda mechi za Seria A tangu mwaka 2011 na imemaliza katika nafasi ya 7, 10 na 8 katika misimu mitatu iliyopita.
Kwa sasa inashikilia nafasi ya 6 katika ligi kuu, alama 20 nyuma ya vinara Juventus.
No comments