Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshi
Source:BBC swahili
Korea Kaskazini imejaribu kufyatua
kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya
Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.
Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.
Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.
Hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani imekuwa ikipanda, huku kila upande ukijigamba jinsi utakavyoweza kuchafua upande mwingine.
Mnamo Ijumaa Uchina iliitisha mkutano unaonuia kutuliza uhasama huo.
No comments