HIZI NDIZO TAARIFA RASMI ZA KUENEA GONJWA LA EBOLA TANZANIA.
Na.Melkiory Gowelle
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
imedhihirisha wazi kwamba mpaka sasa hakuna mtu ambaye amehisiwa kuwa na
ugonjwa wa Ebola na hatuwa za kujikinga na ugonjwa huo unao enea kwa kasi
nchini Kongo zimesha chukuliwa.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekiri kuwepo kwa janga
hilo nchi jirani ya Kongo na kutokana na mwingiliano wa watu ameeleza namna
ambavyo Tanzania imejipanga kukabiliana
na Ugonjwa huo.
“kama mnavyo fahamu ya kuwa Dunia ni Kijiji, hivyo
katika hili ningeomba wasafiri watuvumilie, sababu tumeanzisha ‘Register’ ya
kurekodi wasafiri wa DRC katika vituo vyote vya usafiri, lengo ni kuwafuatilia
wanakotoka, wakoenda na wanapoishi ili kubaini kama wamepatwa na maambukizi au
hapana. Amesema Mwalimu na kuongeza kuwa,
“kwa hiyo wasafiri wa DRC niwaombe radhi kwa kuwa
suala hili ni kwaajili ya kuwakinga watanzania, hivyo tutawaandikisha katika ‘register’
maalumu itakayo ambatana na kujaza fomu maalumu katika vituo vyote vya usafiri
wa anga, majini na nchi kavu.” Amesema Ummy Mwalimu.
No comments