UFUGAJI NG'OMBE WAMTIA MASHAKANI
Source BBC Swahili.
Muislamu mmoja nchini India
amefariki kutokana na majeraha aliopata baada ya kundi moja la wanaume
waliokuwa wakisafirisha ng'ombe kushambuliwa na wanachama wa kundi moja
linalodaiwa kulinda ng'ombe.
Azmat ambaye hutumia jina moja pekee amejifunika nguo , huku akiwa na jeraha la mbavu, damu katika jicho lake la kushoto mbali na majeraha ya kushambuka katika mikono yake na tumbo.
Hatahivyo ana bahati ya kuwa hai.
Azmat pamoja na watu wengine wanne walishambuliwa na walinda ng'ombe wakati walipokuwa wakisafirisha ng'ombe walizonunua kutoka Jaipur katika jimbo la kaskazini la Rajasthan wakielekea katika shamba lao la ng'ombe wa maziwa huko Hiryana.
Licha ya kuwa na vibali halali walitolewa katika barabara kupigwa na fimbo huku umma ukitaka wachomwe wakiwa hai.
''Iwapo polisi hawangefika na kutuokoa sote tungekuwa tumefariki ,aliambia BBC Hindi''.
Ngombe hutambulika kuwa mnyama mtakatifu na raia wa dini ya Hindu walio wengi na kwamba mauaji ya ngombe ni haramu katika majimbo mengi ya India.
Mwezi uliopita ,jimbo la Gujarat lilipitisha sheria inayoharamisha uchinjaji wa ng'ombe na kwamba wanaopatikana wakifanya hivyo watapewa kifungo cha maisha
No comments